Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 3, 2015

Trust Pamoja na Vanessa Mdee Wazindua Rasmi Tamasha la Divas Only Mjini Dodoma...Mwanza na Mbeya Kufuatia


Vanesa Mdee akitumbuiza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha lililopewa jina la “Divas Only Concert” lilifanyika katika ukumbi wa Royal Village na kuratibiwa na Shirika lisilokua la kiserikali DKT International.
Msanii Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.



Ma divas mbalimbali wa jijini Dodoma walijitokeza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililopewa jina la “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika katika hotel ya Royal village jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo liliratibiwa na shirika lisilokua la kiserikali DKT international Trust.
Dodoma 01 Desemba 2015: TRUST, Mwishoni mwa wiki iliyopita TRUST walizindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya Divas Only ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee. Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa ajili ya wanawake. Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye. Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio; Trust iko hapa kukusaidia wakati wa safari hii. Tulifurahia muda tuliopata kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa Dodoma. Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tafuta eneo lilipo Dodoma, Mbeya na Mwanza katika tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!

No comments:

Post a Comment