Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 31, 2015

WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE WAPATA UJASIRI WA KUTUMBUA MAJIPU BAADA YA MAFUNZO YA URAGHABISHI




Ndugu Halidi Abdu toka kijiji cha Shenda chenye wakazi wapatao 2,800 katika kata ya Masumbwi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita;akihojiwa na mtangazaji wa redio free africa william bundala almaarufu Kijukuu cha Bibi k akielezea jinsi walivyoweza kuwaadaa viongozi wao waweze kuwasomea taarifa yao ya mapato na matumizi.
Na Krantz Mwantepele, Geita 
Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje wakati yeye si  kiongozi na ni 

 
jukumu la wanakijiji wote. Katika mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj i r i sha kwa taarifa na maarifa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga hoja mkizithibithisha na vielelezo. Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi na toka kwa nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na maelezo kwa uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenz e n u  k u c h u k u a hatua.”    Baada ya maelezo hayo walitakiwa kwenda kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na baadhi ya maeneo hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri. Maelezo haya yalilenga katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba.

“Kweli mazungumzo hayo yalinijengea uwezo mkubwa sana, Chukua Hatua alinipatia muongozo na akanipangia kwenda kwa mkuu wa wilaya. Moja kwa moja nikaonana na DC nikaanza kumuhoji mambo mbalimbali kuhusu pembejeo. Ingawa majibu aliyonipa sikuridhika nayo, lakini nilishukuru kupata nafasi ya kuongea naye. Na kwa kweli tokea siku hiyo nikawa na ujasiri mkubwa sana,” Fedson Yaida akitoa ushuhuda wa siku ambayo uoga ulimtoka.

Ujasiri huo wenye msukumo wa ndani toka kwa mraghbishi mmoja kwenda kwa wenzake kwa njia ya kuwashirikisha aliyopatiwa na Chukua Hatua, ndio umekuwa chanzo kikubwa cha mafanikio ya pamoja ya wana Shenda katika kusimamia rasilimali zao. Safari ya mwandishi katika kijiji cha Shenda ilimtia moyo sana. Alikutana na waraghbishi toka vijiji vya Shenda, Ipoja, na Buluhe. Mkusanyiko huu ulikuwa na watu wa kada mbalimbali; walimu, wajumbe wa serikali ya kijiji, wazee, na wakulima. Aliwakuta wakiwa pamoja na Mwenyekiti na Mtendaji wa kijiji chao. Na wote kwa pamoja walikuwa wanazungumzia mustakabali wa maendeleo ya kijiji chao. Na kwa haraka aligundua wote wamekuwa waraghabishi, akajiuliza aliyekutana na Chukua Hatua alikuwa mmoja, lakini sasa wapo kwa makundi na wote wanajitambulisha kama waraghbishi.  Hamu na shauku yao ya kutaka kusimamia rasilimali zao ndio imekuwa nguzo kubwa ya wao kuweza kufuatilia matumizi ya vyanzo vya mapato ya kijiji chao. Ni miaka miwili imepita toka wananchi hao wautoe uongozi wa kijiji madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Kwa pamoja waliongozana na mwenyekiti wao pamoja na mtendaji wa kijiji na mpaka ofisi ya kata na kuwakabidhi kwa polisi. Ubadhirifu huo ulithibitishwa na taarifa ya ukaguzi, iliyoonyesha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni mbili laki tisa na elfu hamsini (2,950,000/-). Taarifa hiyo ilisomwa katika mkutano wa hadhara na viongozi kutakiwa kulipa pesa hizo ambazo walizirudisha.

 Waraghbishi toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika pichaya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.

Baada ya hapo walichagua uongozi mpya; mwenyekiti na halmashauri ya serikali ya kijiji na Mkurugenzi wa wilaya akawaletea mtendaji mpya wa kijiji. Na huo ndio ukawa mwanzo mpya wa safari ya uraghbishi katika kijiji hicho. Vuguvugu hilo la mapinduzi liliongozwa na waraghbishi wapya waliowezeshwa na Fedson wakisaidiana na rafiki yake wa karibu Abdu Haridi ambaye pia ni mraghbishi.  Habari ya kutolewa madarakani kwa uongozi wa kijiji hicho ilirushwa pia na redio ya Kahama FM na kupelekea mkuu wa wilaya kumtuma mwakilishi wake akaongee na wananchi wa kijiji cha Shenda.

 Uungwaji mkono huu na Mkuu wa Wilaya ni dalili kwamba yupo tayari kufanyakazi na wananchi wa kijiji cha Shenda. Yeye ni kiongozi wao na dhahiri anawajibika kwao kama ambavyo kiongozi yeyote anayejali watu wake angefanya.   Kwa sasa wanashirikiana kwa pamoja na uongozi mpya na mwandishi alithibitisha hivyo kwa kuwa alipata fursa ya   K a m a mwanzo mpya, wamekubal i ana kufanya ujenzi wa ofisi mpya ya kijiji. 

K wa n z a  wa meanza na ujenzi wa zahanati kwa k u k a m i l i s h a msingi wake. Na wananchi wamekubali kuchangia, kila kaya matofali 50 na wengine w a m e c h a n g i a mawe. Uhai umerudi tena na kila mtu ana shauku ya kufanikisha ujenzi huo. Lakinisi hivyo tu wanataka kukamilisha pia na ujenzi wa zahanati ya kijiji. Haya yote yakiwa ni matunda ya ushirikiano kati ya uongozi wa kijiji na waraghbishi na  wanakijiji wote kwa ujumla.  “Tumekaa muda mrefu sana bila zahanati hasa kwa ajili ya kina mama. Ni kilometa tano kutoka hapa mpaka zahanati ya jirani. Na kijiji chetu kama unavyokijua, hakina teksi, labda tumbebe kwa tela la ng’ombe au punda kama huna baiskeli. Tukajiuliza kwanini tusiiambie serikali yetu tujenge zahanati hapa karibu,”anafafanua Abdi Haridi.  Lakini si hivyo tu Mwenyekiti ameshahamasisha kila mwananchi achangie mawe, achangie matofali. Kwa sasa wameonela kumalizia kabisa ofisi yao ya kijiji. Ya sasa ipo katika hali mbaya harufu ya kinyesi cha popo na jengo lenyewe lina nyufa ikinyesha mvua kubwa itakuwa ni shida inaweza hata kuanguka na hapa ndio makao makuu ya kijiji.

 Kwa hiyo nguvu zao sasa ni kukamilisha hii ofisi afu ndio waendelee na zahanati ya kina mama.  Mazungumzo hayo na Chukua Hatua yalifanyika katika mfumo wa mafunzo  yaliwawezesha waraghbishi toka vijiji vya Ipoja, Shenda, Buluha na Nyakasaluma kuanza kufuatilia na kuhamasisha wengine kufanya hivyo pia.   Si kitu kirahisi sana kuwa mraghbishi, kunahitaji kujiamini, kujitambua na moyo wa kujitolea pia..

  Katika kijiji cha Nyakasaluma wananchi walihamasishwa na uongozi wao kuchangia pesa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na kwa kweli walichangia kila kaya ilitoa kiasi cha shilingi za kitanzania elfu saba mia tano. Swali la kujiuliza michango ya maendeleo ya namna hii, inaamuliwaje? Wananchi wanahusishwaje? Je, wamefanya utambuzi wa watu/kaya/familia uwezo walio nao? Kwa mujibu wa mraghabishi Patrick Matagale ujenzi ulianza lakini ghafla ukasimama na walipofuatilia ikaonekana kwamba ujenzi hautaendelea kwa madai kwamba mwekezaji wa kijiji atamalizia na wananchi pesa wameshachangia.

   “Sasa ilikuwa ni kuhoji tu kuhusu ile pesa iliyochangwa na wananchi”, anasimulia mraghbishi Patrick.  Uaminifu ni silaha kubwa ya uongozi imara, na mara watu wanaposhindwa kukuamini kama kiongozi, huamua kuchukua njia yao ya kutokukupa dhamana ya kuwaongoza,   “Hivyo tulichoamua kufanya kwa sasa ni kwamba hatutachangia tena pesa na badala yake tunahamasisha watu kuchangia vitu badala ya pesa, kama walivyofanya wenzetu wa Shenda. Mwenye mawe, matofali, mbao na chochote kile alete,” anafafanua mraghbishi Patrick Matagale toka kijiji cha Nyakasaluma. 


 Katika kijiji cha Iponya, suala lililoibuka ni michango wanayochangishwa wananchi. Ambapo kila kaya imetakiwa kuchangia kiasi cha shilingi za kitazania elfu sita (6,000/) kwa ajili ya mradi wa maji wa visima virefu. Mradi huu unafadhiliwa na benki ya dunia na una thamani ya shilingi za kitanzania milioni 221/-

Hivyo wananchi nao wametakiwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia pia gharama za ujenzi huo na wananchi walikubali bila kusita na kwa ujumla wao walichangia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu (3,000,000/-).  “Cha kushangaza wananchi wameshachanga hela zao, ila mpaka muda huu naongea hakuna ambacho kimeshafanyika. Lakini kwenye muhadhara tulidanganywa kwamba mradi ukishaanza Shenda na sisi pia tutaanza kufaidika, mpaka dakika hii hakuna maji,” anafafanua Thomas Mlekwa toka katika kijiji cha Iponya.  Wananchi wakawa wanataka kujua nini kimetokea baada ya wao kuchanga, kama anavyosimulia mwana mama Leornada Mathias toka kijiji cha Ipoja, “Ilikuwa mishe mishe kweli, kila siku mwenyekiti anapita katika kaya anahamasisha watu wachangie ili tuondokane na tatizo la maji. 

Ni kweli tuliitikia tukatoa michango na tuliambiwa tukichelewa tu huu mradi unatupita. Tukafungua akaunti na fedha zikawekwa. Baada ya hapo tukaona  kimya kabisa.”  Katika mikutano ya hadhara ya kijiji iliyofanyika hapo wananchi walitaka kujua nini kimetokea kwani fedha tayari kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu zimeshawekwa benki.  

“Kwenye mkutano watu wakataka kujua meza imekuwaje tuliambiwa Shenda wakipata  maji na sisi pia, mbona tayari kwa wenzetu yapo. Ndio tukaja kujua kwamba hakuna mradi wa maji. Na badala yake viongozi wanatuambia kwamba ile fedha wanaanza kuisoma kwenye mapato na matumizi,” anaendelea kufafanua Leornada. 

 Na katika muda huo wakaambiwa kwamba tayari laki nne zimeshatumika kutokana na makato ya gharama za kuendesha akaunti. Kwa hiyo uendeshaji wa akaunti umekula mpaka sasa kiasi cha milioni mbili na laki tatu zimebaki laki saba tu. Hapa pana kazi kubwa ya kufanya.  Pamoja na Shenda kuonekana kwamba kwao maji yameshaanza kutoka katika mabomba, bado kuna changamoto nyingi za kuwezesha kukamilika kwa mradi huo wa maji. Na waraghbishi wapo mstari wa mbele kufuatilia nini kinachoendelea kwenye mradi huo. Ni mradi ambao waliomba wapatiwe na utekelezaji wake umeshaanza ingawa baadhi ya maeneo bado hawapati maji.  

 “Mradi huu wa maji ni sawa na hakuna. Sisi wananchi wa Shenda tumechangia nguvu zetu. Tumechangia asilimia yetu tuliyoambiwa na serikali. Serikali ikachangia asilimia yake, ina maana kilikuwa ni kisima tu cha vitongoji vine vya kijiji chetu. Tuna tenki lile pale limeshakamilishwa.  Mashine ipo kule kwenye chanzo cha maji. Italike kule, lakini kijiji kizima kuna gati nane tu. Kuna vitongoji vingine havina gati. Kitongoji kizima kinapewa gati moja ebu niambie kitakidhi wangapi?” anauliza Abdi Haridi mraghbishi wa Shenda.

Gati zilizopo Shenda zinatokana na waraghbishi na wananchi kufuatilia suala hilo kwa karibu. Kwa sababu ni kitu walichokiomba wapatiwe na serikali. Baadhi ya vitongoji vya kijiji hicho vimetenganishwa na barabara. Hivyo wametaarifiwa kwamba gati haiwezi kuvuka barabara. Ili hali kwa baadhi ya viongozi wao gati imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza,  “Lakini ukienda pale makao makuu ya kata pale unakuta gati imewekwa kwa kiongozi. Nikauliza swali pale mbona kule Shenda tumeambiwa gati haiwezi kukata barabara ndio maana wananchi wa upande wa pili wa kijiji hawapati maji. Imekuwaje kwa kiongozi imekata barabara na kuingia mpaka mgongoni mwa nyumba yake? Barabara ile ile niliyoambiwa gati haiwezi kukatiza ndio hiyo hiyo imetumiwa kukatiza gati.” Kaloras Majura, mraghbishi kutoka kijiji cha Bukandwe kutoka kata yenye jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja na kwamba yeye ni mraghbishi lakini pia alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya kijiji chao.  

 “Changamoto niliyoanza nayo ilikuwa ni pale shule, nilipogundua kwamba mwalimu mkuu anaitisha michango, bila kuwashirikisha wazazi. Pamoja na nafasi niliyokuwa nayo lakini pia nilikuwa natoa elimu kwa wananchi. Nikajengewa kampeni na kufanyiwa uhasama na  mwisho wa siku nikaambiwa nafasi ya uenyekiti hainifai, kwa sababu natoa siri. Hivyo nimebaki mjumbe tu,” katika hali ya upole anaelezea mraghbishi Majura.   

Suala lingine ambalo limejitokeza ni kuhusu mganga wa zahanati ya kijiji cha Bukandwe, ambaye alikuwa akiwachangisha wananchi kiasi cha shilingi za kitanzania elfu kumi (10,000/-) za mfuko wa afya. Alichokuwa akifanya wakati anawaandikia alikuwa akiweka kumbukumbu tofauti za mwaka.  “Kama mtu katoa hela mwaka huu yeye anamuandikia katoa mwaka 2012 na wengine mwaka 2013. Baada ya muda akawa amehamishwa sasa watu wanapokwenda pale zahanati wanaambiwa kwamba wewe muda umeshakwisha ulitoa mwaka juzi hivyo uanze upya,” anasimulia Majura  Kutokana na nafasi yake ya uraghbishi Majura ameweza kukaa na kamati ya kijiji ya afya. Na ameishawishi kamati kuwasiliana na watu waliolipa kuandaa vielelezo vyao na kufanya mawasiliano na mganga mkuu wa wilaya, ili waweze kujua wanachukua hatua gani kuhusu huyo mganga. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanarudishiwa fedha zao walizochanga.

Si kitu kirahisi sana pia kufanya uraghbishi kwa sababu mara kadhaa waraghbishi wamekuwa wakitishiwa tishiwa ili wasiulize ulize maswali na kuhamasisha wananchi , lakini  bado mambo yameendelea.  “Sisi waraghbishi tunapata muda mgumu sana tunakutana na watu tofauti na viongozi tofauti. Tunatishiwa amani, ila na sisi tutapambana kama tulivyokwisha kupambana mpaka dakika ya mwisho ili haki yetu ipatikane. Tukianza kuyatafuta mashirika ili tushirikiane nayo katika kuweka mambo sawa, kama hivi. Tayari tunaonekana siye wabaya kwa wale viongozi wa juu. Kwamba sisi tunawapondea wale. Basi sisi tunaomba waje wale wakubwa zaidi, waje watuulizie nini kinaendelea ili tuwaambie ukweli,” anaeleza kwa kujiamini mraghbishi Abdi Haridi wa Shenda.    Harakati hizi zinaungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Shenda, Masumbuko Kwileka, kama anavyosema kuhusu warghabishi, 

 “Kila siku waraghbishi tunao hapa. Fedson huwa anakujaga hapa wanazunguka huko na kijana wake huyu hapa Haridi. Wanapita vijiji hadi vijiji wanahamasisha.Hivyo waraghbishi wana hamasa hata mwenyekiti ajaye atakayekuja watakuwa msaada kwake. Manake watamuuliza tu sasa mkuu unakwendaje hapa na itabidi uwaeleze mambo yanakwendaje. Hivyo mnapopata pesa ni lazima umuelezee mraghbishi zinavyokwenda.”  Ni mwaka sasa umepita toka shuguli za Chukua Hatua zisimame kwa muda, ila cha kufurahisha ni waraghbishi wameendelea na harakati za kujiletea maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa wananchi wenzao. Na si hivyo tu wameendelea kuwatengeneza waraghbishi wengine ambao na wanaendeleza harakati za kuleta maendeleo.

No comments:

Post a Comment