Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 14, 2016

BACK TO LIFE SOBAR HOUSE: JAMII ISIWATENGE WAHANGA WA DAWA ZA KULEVYA.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Jamii nchini imetakiwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake wawasaidie kuondokana na matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo vya utimamu wa akili (Sobar House).

Rai hiyo ilitolewa wiki hii na Eddy Darkis ambae ni Meneja wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To Life Sobar House kilichopo Pasiansi Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, ambacho kinawasaidia wahanga wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.


Darkis alibainisha kuwa badhi ya wanajamii wamekuwa wakiwanyanyapaa waathirika wa dawa za kulevya, jambo ambalo linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Kwa mwaka 2015, zaidi wahanga 50 wa dawa za kulevya waliokuwa katika Kituo hicho kutoka Mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoani Mwanza, wamerejea katika hali zao za kawaida baada ya kupatiwa tiba ya kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya huku wengine zaidi ya 25 wakiendelea kupatiwa tiba katika kituo hicho.


Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu nchini (OJADACT) Edwin Soko, Idadi ya Watumiaji wa dawa za Kulevya Jijini Mwanza imefikia zaidi ya Watumiaji Elfu Kumi katika kipindi cha miezi sita iliyopita huku sababu za ongezeko hilo zikiwa ni kutokana na kukosekana kwa njia mathubuti za kupambana na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na wanaojihusisha na biashara ya dawa hizo mara kwa mara kubuni mbinu mpya za usafirishaji jambo linalosababisha ugumu katika kupambana na biashara hiyo.

No comments:

Post a Comment