Baraza kuu la uongozi la taifa la chama cha wananchi CUF,
kwa kauli moja limeridhia kutokushiriki
uchaguzi mkuu wa Zanzibar huku likisisitiza kuwa mamauzi ya kufutwa kwa
uchaguzi mkuu wa Oct 25 mwaka jana yalikuwa batili.
Mapema jan 28, baada ya baraza kuu la uongozi la CUF kutumia
saa 4, kujadili agenda moja tu ya kushiriki au kutokushiriki katika uchaguzi wa
mach 20 mwaka huu, makamo mwenyekiti wa CUF taifa akatanagza maadhimio kadhaa
ya kikao hicho.
Miongoni mwa maazimio
hayo 12 ya kikao hicho ni pamoja na ukiukwaji wa katiba ya Zanzibar na sheria
ya uchaguzi namba 11 ya mwaka1984, huku katibu mkuu wa CUF akishutumu kile
alichokiita ni mbinu chafu za kuchafua daktari la wapiga kura mjini Zanzibar.
Aidha tamko hilo
limezitaja jumuiya za SADC, EAC, AU, umoja wa Ulaya, jumuiya ya madola na nchi
za Uingereza na Marekani ambazo amezitaja kuunga mkono uchaguzi wa Oct 25 mwaka
jana, huku likiitaka serikali kutaafkari upya uamuzi wake wa kuitisha uchaguzi
mpya mwezi march.
Haya yanajili baada
ya tamko la mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha kutangaza
kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mapema Oct 28, huku tarehe ya uchaguzi huo wa
marudio ikitajwa kufanyika mapema march 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment