Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Edwaed
Lowassa iliyoko wilayani Monduli mkoani Arusha limeteketea kwa moto na
wanafunzi zaidi ya 70 wa kidato cha kwanza wamelazimika kupewa likizo ya wiki
moja baada ya kukumbwa na hofu iliyotokana na moto huo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw Salum Selemani amesema moto
huo ambao umetekeza mali zote za wanafunzi na majengo unaodaiwa kusababishwa na
hitilafu ya umeme za ulianza saa nne usiku wakati wanafunzi wakiwa darsani na
hakuna aliyejeruhiwa japo baadhi yao walikumbwa na hofu iliyosababisha wapoteze
fahamu na kukimbizwa hosipitali.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya
Monduli ambaye pia ni mkuu wa wilaya Bw Fransis Miti amesema kwa sasa wanafunzi
wote wako salama na wamefikisa hatua ya kuwapa likizo fupi ili waweze kutulia
wakati jitihada kuwawezesha kuendelea na masomo zikifanyika.
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment