Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 18, 2016

PICHA:::WANANCHI WA BONDE LA MKWAJUNI WAFUNGA BARABARA NA KUFANYA FUJO

Hali si shwari hivi sasa katika eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni jijini Dar es salaam, na inaelezwa kuwa baadhi ya Wananchi wamechoma mataili pande zote za barabara na hakuna gari kupita. Jeshi la Polisi lipo eneo la tukio hivi sasa kukabiliana na tukio hilo ambalo chanzo chake unadaiwa ni baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa walikuwa wakazi wa eneo lililobomolewa ambao wameingia barabarani na kufanya fujo. Pia gari la zimamoto limefika eneo la tukio ili kuzima moto huo. (Picha zote na Henry Mdimu)
Endelea kutufuatilia kwa habari zaidi. 

No comments:

Post a Comment