Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 18, 2016

SAHARA MEDIA GROUP YAFUNGUKA BAADA YA TCRA KUVIFUNGIA VITUO VYAKE VYOTE


Kampuni ya Sahara Media Group imetoa tamko lake baada ya wikiendi hii, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, kutangaza kuvifungia vituo vyake vitatu vya redio na runinga kwa madai ya kukiuka agizo la kulipia ada ya leseni.
Vituo hivyo vilivyokuwa kati ya vituo zaidi ya 20 vilivyopewa adhabu hiyo, ni Radio Free Africa, Kiss FM na Star TV.
Katika maelezo yake, uongozi wa SMG umedai kutopewa barua na mamlaka hiyo na kwamba imekuwa ikizingatia ulipaji wa ada za leseni.
“Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatano hadi kufikia mwezi October 2015,” inasema taarifa iliyoandikwa kwenye tovuti ya Star TV.
“Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA na kanda ya Mwanza, makao makuu na Sahara Media Group Limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika. Lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia kutano wa vyombo vya habari bila kujali athari za kufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma. Sahara 


Media Group Limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama,” imeongeza.
“Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki na kuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri Jumamosi na Jumapili sio siku za kazi. Menejimenti ya Star TV inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake, hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa Sahara Media Group Limited na TCRA kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na maridhiano.”

CHANZO: BONGO 5

No comments:

Post a Comment