Ulimwengu wa burudani kupitia shoo za redio umeendelea kubarikiwa vilivyo na kijana DJ Tee kupitia shoo yake ya kila wiki ijulikanayo kama SHUJAAZ RADIO SHOW. Kuanzia Novemba 2015, SHUJAAZ imekuwa ikipasua mawimbi nchini Tanzania kupitia EAST AFRICA RADIO na kudhihirisha uwezo alio nao DJ Tee na kuleta burudani bora kwa vijana.
Kutokana na vijana wengi kuhitaji kuwa sehemu ya SHUJAAZ na kutopitwa na burudani za DJ Tee, vituo vingine viwili vikubwa vya redio vimeamua kumpa shavu DJ Tee na sasa shoo yake itasikiza vizuri mjini Zanzibar na viunga vyake, pia mikoa ya Kusini.
“Ni furaha kuona wengi wana-appreciate kazi yangu. Vijana tujumuike kwenye ndichi ya Shujaaz tusikie vijana wengine wanafanya nini na sisi tujitume ili tutoboe na kutisha zaidi mwaka huu” Alisema DJ Tee.
Kuanzia wikiend hii, mbali na kusikika East Africa Radio, SHUJAAZ RADIO SHOW pia itasikika kupitia CHUCHU FM 90.9 FM mjini Zanzibar (KILA JUMAPILI SAA TANO ASUBUHI) na KINGS FM 104.3 FM iliyopo mjini Njombe (KILA JUMAMOSI SAA KUMI NA MBILI JIONI). Sasa wakazi wa Zanzibar na mikoa ya Kusini watapata nafasi ya kujumuika na ulimwengu wa mashujaa kupitia SHUJAAZ RADIO SHOW.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu SHUJAAZ kwa kujiunga na DJ Tee kwenye mitandao yake ya kijamii, Facebook (http://on.fb.me/1FUl1hX), Twitter (http://bit.ly/1LLGEpK) na Instagram (http://bit.ly/1Hn07t4)
No comments:
Post a Comment