Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 21, 2016

KATIBU MKUU BAWACHA AZINDUA RASMI OFISI MPYA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOANI MWANZA.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele (Kulia). Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza katika Uzinduzi huo, Tendega alipongeza uwepo wa ofisi hiyo ambayo itakuwa ikisikiliza kero za wananchi bila kujalisha itikadi zao za kisiasa kwa ajili ya kupokea hoja za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo kuzisemea bungeni.

"...Kazi ya Mbunge siyo kugawa hela. Kazi ya Mbunge ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Na mimi niseme nitakuwa mwakilishi bora na hapa tumeanza tu ambapo katika ofisi hii nitakuwa napokea na kusikiliza kero za wananchi na kwenda kuzisemea bungeni... Alisema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele.



Ofisi hiyo inapatikana Mtaa wa Ghana Green View, Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza. Ndani yake pia kuna Ofisi ya BAWACHA Mkoa wa Mwanza.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele. Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akiwa pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Mwenye Kinasa sauti ni Damas Kimenyi ambae ni Katibu wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema), akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Madiwani wa Chadema Mkoani Mwanza wakijitambulisha wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Akina mama wa Chadema wakiwa katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Bendera za Taifa na Chadema zikipandishwa wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Akina Mama wa Chadema Mkoani Mwanza wakimlaki Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega wakati wa Uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Kabla ya Uzinduzi huo, Kulikuwa na Shughuli ya Kuwatembela wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. BONYEZA HAPA Kutazama ilivyokuwa.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

No comments:

Post a Comment