Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, February 17, 2016

MWENYEKITI WA BODABODA MKOANI MWANZA ATOA TAHADHARI JUU YA VITENDO VYA UKWAPUAJI JIJINI MWANZA

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda (pichani), amewataharisha wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa makini wawapo barabarani, ili kuepukana na vitendo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu kwa kutumia pikipiki.

Kayanda alitoa tahadhari hiyo jana Jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya ukwapuaji vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya waendesha pikipiki, jambo linalochafua taswira ya waendesha pikipiki Mkoani Mwanza.

Tayari watu kadha wamefikisha malalamiko yao kwa uongozi wa bodaboda Mkoani Mwanza, baada ya kukumbwa na kadhia ya kukwapuliwa mikoba pamoja na mabegi yao, ambapo mmoja wa wahanga wa matukio hayo Diana Abdallah ameeleza kukwapuliwa mkoba wake uliokuwa na pesa pamoja na vito vya thamani wakati akitokwa kwenye shughuli zake.


"Nilikuwa maeneo ya Nyegezi ambapo nilikuwa nikitoka kwenye shughuli zangu, nilikwapuliwa mkoba wangu ambao ulikuwa na pesa shilingi Laki Nane, Simu ya shilingi Laki mbili na nusu, Pete sita za Silver zenye thamani ya shili laki moja na elfu ishiri na sita pamoja na miwani ya macho ya shilingi Laki nne. Watuhumiwa waliweza kukamatwa na kesi iko polisi katika kituo cha Igogo".Alisema Abdallah

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu nchini Edwin Soko, analaani Vitendo hivyo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi ya watu kwa kutumia bodaboda ambavyo vimekuwa vikiwakumba watembea kwa miguu Jijini Mwanza, ambapo ameomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano wake kwa ajili ya kuvikomesha.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

No comments:

Post a Comment