Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, February 17, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE DK HAMISI KIGWANGALLA WATEMBELEA MUHIMBILI


 Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamisi Kigwangalla wakikagua wodi mpya ya wazazi ambayo awali ilikuwa ofisi za kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo.

 Waziri Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wa figo waliolazwa katika jengo la watoto. 
 Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa watoto wanaougua ugonjwa wa saratani waliolazwa katika jengo la watoto lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).


 Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi, Aksante wakati akimwelezea juhudi zinazoendela za kukarabati jengo la watoto ambalo lipo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya Rais John Pombe Magufuli kuaagiza. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akimsikiliza mkururugenzi huyo. Leo Waziri Mwalimu na naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Kigwangalla wametembelea Jengo la Watoto na Jengo namba mbili la wazazi kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye ametaka jengo la watoto linalovuja likarabatiwe haraka.
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamisi Kigwangalla wakitazama jengo (pichani halipo) ambalo limeaanza kukarabariwa baada ya agizo la Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Picha zote na John Stephen-Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- kwa lengo la kukagua jengo la watoto pamoja na jengo la wazazi namba mbili ( Maternity Block Two) ili kuona utendaji kazi na utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli . 
 Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Magufuli aliagiza watumishi wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , wazee na Watoto kitengo cha afya ya mama na mtoto kuhama katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa Muhimbili kulitumia kama wodi ya wazazi . 
 Waziri Ummy ambaye ameambatana na Naibu Waziri Dokta Hamis Kigwangala ameelezea kuridhishwa na ukarabati unaoendelea katika majengo hayo . 
“Jengo la watoto tatizo kubwa lilikuwa ni miundombinu ya maji lakini naona ukarabati unaendelea vizuri na nina imani kuwa ukarabati utakamilika kwa wakati” amesema Waziri . Akizungumzia kuhusu jengo la wazazi namba mbili.
Waziri huyo wa afya amesema kuwepo kwa jengo hilo ni faraja kwa kina mama na kusisitiza kwamba hakuna mama mjamzito atakayelala chini . Mpaka sasa kina mama 53 tayari wamehamia katika jengo hilo na wanapatiwa huduma zote.

No comments:

Post a Comment