Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, March 4, 2016

DK.KIGWANGALLA AFUNGUA RASMI JENGO LA WAGONJWA MAHUTUTI MUHIMBILI.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru (kushoto) akisoma hotuba maalum juu ya uzinduzi huo wa wadi ya wagonjwa Mahututi (ICU). Anayefuatia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi. Wengine ni wadau waliowezesha kwa wodi hiyo akiwemo Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya tumbo kutoka Misri, Prf. Abdel Meguid.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo katika mkutano huo wakati alipokuwa mgeni rasmi mapema  Machi 3.2016.

 
Dk. Kigwangalla akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wadi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika jengo la Mwaisela. Wanaoshuhudia ni Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kulia) na Prf. Museru kushoto.
 (Picha zote na Andrew Chale.)
SERIKALI imesema kwa sasa itakuwa ikihudumia wagonjwa wote ndani ya nchi ikiwemo wale wagonjwa Mahututi ambao awali walikuwa wakipelekwa nje ya nchi. Hii ni baada ya kuendelea kuimarisha huduma hizo pamoja na kuwa na wataalam wa kutosha ambaio watapatiwa mafunzo zaidi.

Kauli hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kuzindua rasmi wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliyopo katika jengo la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Dk.Kigwangalla katika uzinduzi huo, amewapongeza watendaji wote waliofanikisha ikiwemo uongozi uliopita na ule wa sasa, Serikali pamoja na wadau wa sekta hiyo ya afya walioguswa na kuchangia upanuzi wa huduma za tiba ya wagonjwa hao Mahututi ambayo imewezeshwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa huku ikiongezwa vitanda kutoka 8 hadi 25 kwa sasa.

Aidha, Dk. Kigwangalla ametoa shukrani ya kipekee kwa wadau waliojitolea kwa moyo wao kuchangia huduma hiyo ya wagonjwa Mahututi ikiwemo Shirika lisilo la Kiserikali la Gastrenterology Foundation kutoka Ujerumani na wadau wote kwa kuweza kufanikisha huduma hiyo kuweza kupatikana hapa nchini na kupunguza safari za nje ambazo zimekuwa zikiigharimu Nchi fedha nyingi.

No comments:

Post a Comment