Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 7, 2016

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. BALOZI ENG. JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wakwanza kushoto na Wamwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. 

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na viongozi Wakuu wa Ulinzi na Usalama nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu.

Balozi Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini.

Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi.

Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.

Hata hivyo amesema idadi ya wakimbizi wanaokimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa.

Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania.
Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

07 Machi, 2016

No comments:

Post a Comment