Na Baraka Mpenja Dar es salaam 0712461976
MBEYA CITY FC kwa mara ya kwanza imepata udhamini wa
mamilioni ya fedha baada ya Kampuni ya Binslum Tyre Company Limited kumwaga
kitita kirefa cha milioni 360 kwa miaka miwili.
Kampuni hii ina nia ya kuifanya klabu hii kuwa bora zaidi
katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara . Siku zote ukifanya kazi kwa
moyo wote, ukawekeza nguvu kubwa kutafuta mafanikio, mwisho wa siku juhudi zako
zinakulipa.
Msimu uliopita, Mbeya City walionesha nguvu kubwa na mipango
mizuri ya ndani na nje ya uwanja. Walicheza kwa kujituma, kwa malengo na
nidhamu kubwa. Timu hii ilikuwa bora kuliko timu zote tatu zilizopanda ligi kuu
kwa msimu uliopita.
Ashanti United na Rhino Rangers ziliishia kuonja tu utamu wa
ligi kuu na kurudi tena ligi daraja la kwanza. Lakini kwa Mbeya City fc ilikuwa
ni tofauti, walishindana mpaka dakika ya mwisho na kumaliza katika nafasi ya
tatu.
Waliwachomoa wakongwe, Simba sc katika ushindani wa nafasi
tatu za juu. Nidhamu ya wachezaji na kuwa na uchu wa mafanikio, maandalizi ya
muda mrefu, falsafa ya kocha Juma Mwambusi, hamasa ya mashabiki, uongozi wenye
mipango, ni miongoni mwa sababu chache kati ya nyingi zilizowafanya Mbeya City
wafike pale walipo.
Lakini kilio chao kilikuwa ni kukosa udhamini. Viongozi
walisikika mara nyingi wakisema wanaomba makampuni mbalimbali kujitokeza
kudhamini klabu. Haikuwa rahisi kupata udhamini kwasababu ndio kwanza watu
walikuwa wanapima upepo wake.
No comments:
Post a Comment