Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 21, 2011

DIAMOND AMWAGA WEMA SEPETU


Musa Mateja na Imelda Mtema
NGOMA ikilia sana ujue inakaribia kupasuka na lisemwalo lipo kama halipo, basi li njiani laja! Hatimaye Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, wamemwagana rasmi, The Udaku Master, Ijumaa lina ‘eituzedi’ ya mkasa mzima.
Ilikuwa ni Jumanne, saa mbili usiku, Diamond ‘Platinum’ aliita vyombo vya habari katika Hoteli ya Lion Sinza jijini Dar es Salaam na kufunguka:
“Washikaji, nimewaita hapa nifunguke mbele yenu kuwa nimemmwaga rasmi yule demu (Wema) kwa sababu hapatani na mama yangu (Sandra Sammy).

ALINILAZIMISHA NITENGANE  NA MAMA
“Kwanza Wema amekuwa akinilazimisha nitengane na mama yangu, yaani nimrudishe kule Tandale tulipokuwa tukiishi mwanzo , halafu mimi na yeye tuishi Sinza (Madukani), jambo ambalo sipo tayari kulifanya.
“Mimi na mama tumetoka mbali, hakuna kama yeye, alikuwa akishinda njaa ili mimi nisome, alinilea kwa shida sana, hata siwezi kuelezea kwani nikikumbuka huwa natokwa machozi, kwa hiyo siwezi kumtelekeza kwa sababu ya Wema.
“Hata katika muziki, nakumbuka nilishamuibia pete yake ya dhahabu nikaenda kuiuza ili nirekodi muziki na alinivumilia.
NI WAKATI WA MAMA ‘KUINJOI’
“Piga ua, huu ni wakati wa mama yangu kula na ‘kuinjoi’ matunda ya mwanaye, mapenzi hayawezi kusababisha nimtende vibaya. Natamka rasmi huyu demu nimemmwaga bwana.”
SWALI LA MWANDISHI WA IJUMAA
“Mlianza mapenzi muda mrefu na ni wiki mbili tu zimepita tangu ulipomvisha pete ya uchumba, je, hukujua kwamba mambo kama haya yangetokea?
DIAMOND AKAJIBU
“Sikuligundua hilo mapema na pia si unajua mambo ya ujana tena? Ukweli ni kwamba tukio hili limenikumbusha kuwa ujana ni jalala linalotupwa kila aina ya takataka.”
UPANDE WA WEMA
Baada ya Diamond kumwaga unga na ishu hiyo kuwa gumzo jijini Dar usiku kucha, kama ilivyo desturi ya gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa nchini, asubuhi na mapema (Jumatano), mapaparazi wake wa kuheshimika walimsaka Wema ili kupata mzani wa habari hiyo.
NDANI YA HOTELI YA LAMADA
Kutokana na uzito wa habari yenyewe, Ijumaa lilisaga lami hadi Hoteli ya Lamada Ilala, chumba namba 35 flati ya Mikumi ambapo Wema alikuwa kambini kwa ajili ya kurekodi filamu.
HALI ILIKUWA HIVI
Baada ya kubisha hodi, ‘mkaribisha wageni’ alikuwa  Elizabeth Michael ‘Lulu’, alifungua mlango ambapo Wema alishuhudiwa akinyanyuka na kwenda kuosha uso, aliporejea na kuwaona ‘polisi’ wa Ijumaa wakifunga ‘makamera’ yao alipaza sauti na kufuatiwa na kilio: “Maweee! Nimeachwa? Nyiii….nyiiiii.”

Lulu: Nyamaza Wema usikie kilichowaleta.
Ijumaa: Mambo vipi Wema?
Wema: Hata salamu yenu sitaki, niambieni nimeachwa?
Ijumaa: Poa, ili mgonjwa apone lazima achomwe sindano inayouma au ameze vidonge vichungu. Iko hivi Wema; jana pale Lion Hotel, Sinza,  Diamond alitangaza rasmi kukutema kwa sababu eti umekuwa ukimlazimisha kumtenga mama yake ili muishi peke yenu, yeye hayupo tayari kufanya hivyo, je, hili unalizungumziaje?


Wema: (kilio) siko tayari kuzungumza chochote.
Ijumaa: Tafadhali waambie mashabiki wako umeipokeaji taarifa hii?

Wema: Amenidhalilisha, nitaweka wapi uso wangu? Anyway, niacheni nitawatafuta baadaye niongee.
Lulu: Dada Wema, funguka tu kile unachokijua, itakusaidia watu wajue ukweli.
Wema: No, please. Waondoke tu nitawatafuta baadaye.


UTABIRI
Ili kuthibitisha kuwa kile kinachoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kina uhakika asilimia zote, wakati hayo yanatokea, tayari gazeti tumbo moja na hili, Risasi Mchanganyiko toleo namba 844 la Jumatano wiki hii lililokuwa na kichwa cha habari: WEMA, DIAMOND HAKUNA NDOA, lilitabiri na kuweka vigezo kuwa Wema na Diamond hawatadumu.

Aidha, Gazeti la Risasi Jumamosi iliyopita, ukurasa wa 16 kulikuwa na habari yenye kichwa; ETI WEMA, MAMA MKWE WAKE HAWAIVI.
Diamond alionesha kutokubaliana na madai hayo, lakini yaliyotokea yameweka wazi.


WADAU WANASEMAJE?
Kwa mujibu wa wadau walioinyaka habari hiyo walilieleza Ijumaa kuwa haijawahi kutokea Wema akamwagwa na midume kwani yeye ndiye huwa anawamwaga.
“Ama kweli mtenda akitendewa…safari hii kaachwa yeye!” alisema mmoja wa wadau hao.


ANATAMANI DUNIA IRUDI NYUMA
Uchunguzi wa Ijumaa ulibaini kuwa usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii, Wema hakupata usingizi kwa kuwa alishanusa dalili za tukio hilo.

“Ukweli Wema hakulala kabisa, alikuwa akijigeuza mara kwa mara na kutaja jina la Diamond huku akilia, alipoulizwa kulikoni alijibu: “Natamani dunia irudi nyuma ili lile tukio la kuvishwa pete ya uchumba pale New Maisha Club wiki mbili zilizopita lifutike,” alisema mmoja wa wasanii aliyekuwa naye kambini hapo.

No comments:

Post a Comment