Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 21, 2011

Sugu anusurika kifo ajalini











MSANII mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini, Joseph Mbilinyi ‘Mr II au Sugu’ (pichani), juzi amenusurika kifo kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea katika eneo Vibwabwa mkoani Iringa.

Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), alinisubirika kifo baada ya gari lake aina Toyota Land Cruiser kuligonga roli lililokuwa limeharibika na kuegeshwa barabarani bila ya alama yoyote.

“Kweli tunamshukuru  sana Mungu, maana gari limeharibika vibaya sana. Mbaya zaidi baada ya sisi kunusurika, saa chache baadaye tumeambiwa kuna Toyota Corolla imeliingia lile roli na kuua watu watatu pale pale,” alisema Sugu hiyo jana.

Sugu alinusurika katika ajali hiyo wakati akiwa njiani kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam. Ndani ya gari alikuwa pamoja na msanii mwingine Fred Marik maarufu kama Mkoloni pamoja na DJ mkongwe wa mjini Mbeya aitwaye BBG.

Kabla ya kuukwaa ubunge, Sugu alitoa mchango mkubwa kukua kwa muziki wa kizazi kipya hasa upande wa miondoko ya Hip hop aliyoitangaza Afrika, Ulaya na Marekani.

No comments:

Post a Comment