MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson
amewathadhalisha wachezaji wake kuwa katika kiwango cha juu
watakapowakaribisha mahasimu wao Manchester City kwenye mchezo
utakaowakutanisha vinara hao wa ligi hapo Oktoba 23.
Mabingwa
United na City zinafungana kwa pointi, na United inaongoza kwa tofauti
ya bao moja tu.Kocha huyo mwenye miaka 69, ambaye amewaita majirani zao
hao kuwa 'wapinga kelele', alisema hakushangazwa na City walivyoanza
msimu kwa kishindo.
"Nilishasema kabla kwamba hili litatokea,"
Ferguson aliliambia gazeti la klabu hiyo Jumanne iliyopita."Wanatimu
nzuri ya kuwafanya kuendelea kubaki kwenye nafasi ya juu.
"Sergio
Aguero amekuwa na mafanikio tangu alipotua katika Ligi Kuu, kwa sababu
anauwezo mkubwa wa kufunga na ni mchezaji hatari kwenye eneo la
penalti. Pia, David Silva ni mchezaji mzuri.
"Tunachotakiwa ni kuhakikisha tunakuwa tayari kwa ajili ya City wakati tutakapokutana nao."
Timu
zote United na City hawajapoteza pointi katika Ligi Kuu msimu huu,
wakiwa na rekodi ya kushinda mechi sita na kutoka sare moja, na
Ferguson amekiri mechi ya watani wa jadi imebadilika tangu alipoingia
bilionea Sheikh Mansour wa Abu Dhabi.
"Mechi zote za mahasimu ni
kubwa sasa, hakuna mchezo rahisi," alisema Ferguson."City sasa ni timu
kubwa, imefanya usajili wa nyota bora na ukiongeza fedha zao za kuvutia
wachezaji wengi bora duniani hiyo ndiyo iliyobadilisha mechi hii hivi
sasa.
"Kupata pointi si kitu muhimu sana katika mchezo, lakini
jinsi Manchester City walivyoweza kubadilisha soka na ndicho
tunachotakiwa kushindana kwa hilo."
No comments:
Post a Comment