skip to main |
skip to sidebar
MAULID HAMAD MAULID AMETUACHA WAPWEKE WANATASNIA YA HABARI
CHAMA Cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (Taswa), kinasikitika kutangaza kifo cha
mwandishi mahiri wa habari za michezo Zanzibar, Maulid Hamad Maulid.
Maulid
ambaye anafanyia kazi vituo vya Redio One na ITV akiwa Zanzibar,
amefariki dunia leo Jumanne Oktoba 18, 2011 asubuhi nyumbani kwake
Jang’ombe Zanzibar.
Taswa imepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kifo cha Maulid kwani alikuwa kiungo muhimu kwa ushirikiano
kati ya Taswa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar.
Pia
Maulid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Taswa Zanzibar ambayo ilianzishwa
hivi karibuni kwa lengo la kuwaweka pamoja waandishi wa habari za
michezo Zanzibar.
Tumepoteza mtu muhimu, mpiganaji mahiri katika mambo ya michezo ambaye daima Taswa tutaendelea kumkumbuka.
Tunaipa
pole familia yake, Taswa Zanzibar na wanamichezo wengine weote kutokana
na msiba huo mkubwa na tupo nao katika kipindi hiki kigumu.
Wakati
wa uhai wake Maulid licha ya kuwa kiongozi wa timu mbalimbali ikiwemo
kuwa Rais wa timu ya Taifa Jang’ombe iliyopata kushiriki Ligi Kuu
Zanzibar, pia amepata kuchezea timu ya Kikwajuni ya Zanzibar.
Pia amepata kuwa msemaji wa Chama cha Soka Zanzibar(ZFA) kabla ya kujiondoa baada ya uchaguzi wa chama hicho mwaka jana.
Kulingana
na taarifa ambazo Taswa imezipata kutoka kwa Katibu wa Taswa Zanzibar,
Donisya Thomas ni kuwa taratibu za maziko zilikuwa zikiendelea na kuna
uwezekano mkubwa akazikwa leo alasiri. Mungu aiweke mahali pema peponi
roho ya Maulid Hamad Maulid.Amin
Amir Mhando
Katibu Mkuu Taswa
No comments:
Post a Comment