Uongozi wa klabu ya Simba kupitia mwenyekiti wake Aden Rage umesema
suala la mchezaji wao Kelvin Yondani ambaye anatuhumiwa kwa utovu wa
nidhamu, na kupewa barua mbili na ambazo hakujibu hata moja, sasa
uongozi wa Simba pamoja na kamati ya ufundi umemtaka aje azungumze nasi
kama anataka kuvunja mkataba na wako tayari.
Alisema
kuliko kitendo cha kuongea na vyombo vya habari ni bora aende
kuzungumza na uongozi na wao watamruhusu kama atahitaji kuondoka,
kuliko kukaa kimya bila ya sababu.
Aliongeza
kuwa kutokana na kosa la Yondani, wangeamua kuchukua hatua kwa kufuata
kanuni za FIFA na za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingemwia vigumu
mchezaji huyo, kwani mchezaji akiwa na kosa la utovu wa nidhamu,
anastahili kufukuzwa na haruhusiwi kwenda kujiunga na klabu yoyote
mpaka uongozi wa timu husika aliyokuwa anaichezea ukubaliane na hilo.
No comments:
Post a Comment