Mfalme kutoka kaskazini, staa wa single ya bye bye rappa Joh
Makini amezungumza exclusive kwenye amplifaya jana baada ya kauli
iliyotolewa na uongozi wa studio ya B HITS iliyohusika kuitengeneza hiyo
single ya bye bye.
boss wa b hits music group Hermy B, aliandika jana kwenye
facebook kwamba “Joh Makini umeikasirisha B’Hits, Wimbo wa bye bye
tulikupa bure baada ya kutujibu kwa dhihaka tulipodai malipo yetu, Hata
kutupa Credit zetu kwenye video umeona kazi pia, ama kweli shukrani ya
punda ni mateke, we mtu gani? Kumbuka ulipotoka!!!
Hizo ni lawama kwamba, audio ya bye bye ilitengenezwa na b
hits lakini kwenye video iliyotengenezwa na Adam wa Visual Lab, B hits
haikuandikwa kama ndio imehusika kuitengeneza.
Joe Makini akizungumza na AMPLIFAYA ya Millard Ayo, amesema
“sidhani kama kuna matatizo yoyote kati yangu na B HITS kwa sababu hata
jana nilikua na Producer wao PANCHO LATINO, na kilichotokea ni bahati
mbaya tu Adam hakuandika B HITS kwamba ndio wamehusika kuitengeneza hiyo
AUDIO, hata hivyo sisi wenyewe hatukutegemea kama ingekua kitu kikubwa hivi na kuleta mvutano mkubwa kama huu, ni kitu ambacho ni cha kurekebishwa tu kirahisi” – JOH MAKINI
amemalizia kwa kusema nimeanza kusambaza
video ya bye bye ambayo tayari Adam ameshaifanyia marekebisho na
kuiandikia jina la B HITS, kuanzia leo na kesho ndio hiyo kazi ya
kuzisambaza inafanyika.
Waziri Jafo akagua maandalizi miaka 60 ya CBE
-
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo ametembelea Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) kuangalia maandalizi ya sherehe za miaka 60 t...
41 minutes ago
No comments:
Post a Comment