Gardner habash, mume wa mwimbaji lady Jay d ametoa taarifa kuhusu
mgahawa wao wa NYUMBANI LOUNGE kufanyiwa shambulizi na mtu ambae
hajafahamika mpaka sasa, ambae lengo lake lilikua kuharibu biashara
ijumaa ya weekend iliyokwisha jana.
amesema “ilikua ghafla sana ijumaa usiku kwenye saa 7 au 8,
na aliyefanya hilo jambo baya alifanya kwa haraka sana ili watu
wasimuone, bahati mbaya sana ilikua ni muda ambao watu
wamekaa wanaenjoy muziki wa machozi band, tulisikia tu kuna harufu kali
ndio watu wakasema itakua ni PAPER SPRAY, uzuri ni kwamba watu
hawakuchachawa, tulifungua milango ambayo ni mikubwa watu wakatoka
kirahisi na baada ya harufu kuondoka watu wakarudi na kuendelea kuenjoy”
– GARDNER
Habash amesema ukiacha tu uharibifu wa
biashara, kitendo kilichofanyika ni hatari pia kwa afya ya binadamu,
alafu biashara kama hii utasema uiharibu leo lakini kuna watu waelewa na wanafaham imefanyika kwa makusudi kwa hiyo huwezi kuwaondoa watu sehemu wanayoipenda kwa sababu umetupa vitu vichafu.
mpaka sasa mtu aliyeitupa hiyo spray bado hajafahamika ila lengo lake limefahamika, kwamba ni kutaka kuraribu biashara.
MATUKIO; MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA TAWJA
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha Majaji na
Mahakimu ...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment