KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUDHAMINI MASHINDANO YA KOMBE LA CECAFA TUSKER CHALLENGE KWA 823/- MILIONI.



Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries
limited (SBL), kampuni inanyokua kwa kasi hapa nchini, kupitia bia yake
ya Tusker, leo wametangaza udhamini kwa mashindano ya kombe CECAFA
Tusker Challenge mwaka huu.
Udhamini huu ni wa kiasi cha fedha za kitanzania shillingi milioni 823. Fedha
hizi zitagharamia mahitaji kama vile: tiketi za ndege kwa msafara wote
wa CECAFA pamoja na wahusika wakuu wa CECAFA, malazi, usafiri wa magari
hapa nchini, watoa
huduma, fedha za washindi, malipo ya CECAFA ndani na nje ya nchi. Kodi
ya uwanja wa mpira, ulinzi na sehemu za mazoezi kwa wachezaji. Hali kadhalika, fedha hizi zitatumika kuratibu waandishi wa habari na mahitaji mengine ya utawala. Mashindano haya yanategemewa kuanza tarehe 25 Ocktoba hadi tarehe 10 Disemba 2011.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhiana hundi ya udhamini huo,
iliyofanyika jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa SBL Bw. Richard
Wells, alisisitiza kwamba hii ni
mojawapo ya malengo yaliyowekwa na kampuni hiyo yakiwa na nia ya kukuza
nakuendeleza mchezo huu nchini. Vile vile kukuza na kuinua vipaji vilivyopo mashariki na magharibi mwa
Afrika. Udhamani huu unadhihirisha msimamo wa SBL kuwa kampuni
inayowajibika kwa jamii inayoizunguka nchini na nchi jirani za kiafrika.
‘Tunatengeneza Tusker nchini Tanzania sasa, na kinywaji hiki kinapatikana katika eneo zima la Afrika Mashariki. Tunajivunia
kuwa wadhamini wakuu wa CECAFA na tunashukuru kupewa heshima hii na
CECAFA pamoja na TFF’. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa kampuni ya bia
ya Serengeti kudhamini mashindano haya. Mwaka jana, ilitumia kiasi cha shilingi milioni 675, ambapo timu ya Taifa, Tanzania bara Kilimanjaro stars iliubuka mshindi.
No comments:
Post a Comment