,DALADALA MKOANI MARUSHA ZAGOMA KUFANYA SHUGULI ZA USAFIRISHAJI KWA MASAA SITA.

Na Gladness Mushi,Arusha
Hali ya jiji la Arusha imeingia doa kubwa mara baada ya kuwepo kwa mgomo wa daladala ambao umedumu kwa masaa sita kutokana na kile kinachodaiwa kuwa Chadema wamekuwa wakinyimwa haki za msingi .
Mgogoro huo ambao umesababisha madhara makubwa kwa mkoa wa Arusha hasa Leo kwa kuwa
madereva wa daladala nao walisitisha safari zao za kubeba abiria kwa
muda hali ambayo ilizua tafrani kubwa sana ndani ya jiji.
Bw. Ephata Nanyaro
ni mwenyekiti wa vijana kwa mkoa wa Arusha ambapo alisema kuwa hali
hiyo ni mfano tu lakini itadumu endapo kama serikali itaendelea
kuwapuuzia masuala yao mbalimbali ambayo wanataka yatekelezwe.
Aidha Bw Nanyaro aliendelea kwa kusema kuwa mara
nyingi wamekuwa wakitoa maalamiko yao lakimi yamepuuzwa kwa kiwango cha
hali ya juu amba moja ya hilo ni pamoja na mgogoro baina yao na mkuu wa
polisi wilaya ya Arusha bwa zuberi Mwombeji.
Nanyaro
alisema kutokana na kupuuzwa kwa madai yao mbalimbali kumeasabaiusha
hali ya leo ya jiji la Arusha kukosa usafiri ambapo magari ya kubebea
abiria katika kona zote nayo yaligoma kufanya kazi kwa mashinikizo hayo.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha Bw Mwombeji alipoulizwa juu ya tuhuma hizo ambazo zinaelekezwa kwake na chadema alikana juu ya shutuma hizo na kudai kuwa yeye hayupo hivyo
“ieleweke wazi kuwa mimi ni mtu mzima na kamwe kinachosemwa na Chadema si cha kweli ila wana mpango wa kunichafulia jina tu hamna kitu kingine"alisisitiza Bw Mwombeji
Kutokana
na hali hiyo Daladala za mji wa Arusha hazikuweza kufanya kazi na kutoa
huduma za usafiri ambapo mgomo huo wa kushinikiza kuonewa kwa chama
hicho na mbunge wa Arusha mjini Bw Goodbless Lema ulidumu kwa zaidi ya
masaa sita huku daladala ambazo zilijaribu kufanya shuguli zake
ziharibiwa na kuvunjwa vibaya na baadhiya watu ambao wanashinikiza juu
ya kumkataa OCD na kupinga juu ya kuonewa.
Hata
hivyo taarifa mbalimbali zizlizotolewa na na baadhi vyombo vya habari
zilisema Mbunge wa Arusha mjini Bw. Godbless Lema amekwenda Rumande,
mara baada ya kukataa dhamana hukiu wenzake wakiachiwa kwa dhamana
katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kuitisha maandamano bila kibali cha
Polisi.
No comments:
Post a Comment