Mfugaji
Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama
ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser lenye
nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa
Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada
ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha
hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya
shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo.
Gari
aina ya Toyota Landcruiser lenye nambari ya usajili T 566 BQH.
iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani
Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein na kisha kumgonga ng'ombe mwenye
thamani ya laki 6 na kisha kufa papo hapo, baada ya kuwakosa wafugaji
hao baada ya kujistiri nyuma mti.
Jeshi
la polisi lilifika eneo la tukio na kushuhudia ng'ombe huyo akiwa
amefariki lakini hawakuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya
mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry
Baquzein, aliyetumia gari lake kufanya mauaji ya ng'ombe huyo.
Wafugaji
wakionesha jinsi mwekezaji huyo alivyokuwa akiwakimbiza na pichani ni
alama za magurudumu ya gari yalipopita wakati akiwafukuza.
Sehemu ya shamba ambayo mwekezaji wa Kapunga Rice Project ameshindwa kuilima na nyasi zikiendelea kuota.
Moja
ya mitambo inayotumika katika shughuli katika shamba hilo la Kapunga
Rice Project ikiwa imeachwa katika moja ya sehemu ya shamba ambayo
mwekezaji ameshindwa kuilima, na nyasi kuendelea kuota.
Baada
ya mwekezaji wa Kapunga Rice Project kufunga njia zinazoingia na
kutoka, pia kufunga maji ya bomba wananchi wa kijiji cha Kapunga wapo
katika hatari kubwa kama inavyooneka pichani, wanawake wakivuka kuelekea
ng'ambo ya pili kwa kutumia gogo.
(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)
No comments:
Post a Comment