Mcheza kandanda bora
mara mbili barani Afrika, Rashidi Yekini amefariki dunia.Yekini
alizaliwa katika jimbo la Kaduna mwaka 1963. Baada ya kuanza kucheza
kandanda ya kulipwa kwenye ligi nchini Nigeria, alikwenda Ivory Coast
kuichezea klabu ya Africa Sports. Baada ya hapo alitimkia Ureno ambako
alikuwa mfungaji mabao hodari katika ligi ya daraja la kwanza ya Ureno
ambapo msimu wa 1993–94 alikuwa amepachika mabao 34 katika mechi 32
alizocheza.
Kupanda kwa kiwango
chake cha usakataji kabumbu akiichezea timu ya taifa ya Nigeria msimu
huo ambapo Nigeria ilishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kombe la
Dunia na baadae kufuatiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika, alitunukiwa
tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 1993, akiwa mchezaji wa kwanza wa
Nigeria kupata tuzo hiyo.
Rashid Yekini, ambaye
alikuwa ametalikiana na mkewe tangu mwaka 1994 alikuwa akiishi maisha
ya tabu na wapangaji wengine wachahe katika nyumba yake mjini Ibadan,
jimbo la Oyo ambapo iliarifiwa mara chache sana alikuwa akitembelewa na
wageni.
Yekini amefariki
dunia akiwa na umri wa miaka 49. Ameacha watoto wawili. Anazikwa siku ya
Jumamosi kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu huko Irah, jimbo la
Kwara.
No comments:
Post a Comment