ASEMA FIGO ZAKE ZIMESHINDWA KAZI, ZATAKIWA DOLA 40,000 KUMPELEKA INDIA
AFYA
ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka
imebadilika na kuwa mbaya, baada ya figo zake kushindwa kufanya kazi ya
kuchuja sumu ya mwili na kusababisha apatiwe huduma ya kusafisha damu
yake.
Habari
zilizopatikana jana na kuthibitishwa na kiongozi wa jopo la madaktari
wanaoendelea kumtibu, Profesa Joseph Kahamba, zilieleza kuwa hali ya Dk
Ulimboka ilibadilika na kuwa mbaya na hivyo kuwapo mikakati wa
madaktari wenzake kukusanya fedha ili kumpeleka nje ya nchi.
Dk
Ulimboka ambaye amelazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji
Uangalizi Maalumu (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alipatiwa
huduma hiyo jana asubuhi kwa kutumia mashine maalumu, iliyoko katika
Kitengo cha Watoto cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Daktari
huyo ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari unaoendelea nchi
nzima kutokana na Serikali kushindwa kutimiza madai yao mbalimbali,
amelazwa kutokana na majereha aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za
mwili, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, kisha kupigwa,
kung'olewa kucha, meno mawili na kutupwa katika Msitu wa Pande, usiku
wa kuamkia Jumatano.
Tangu
alazwe MOI baada ya kuokotwa na wasamalia wema, katika Msitu wa Pande
uliopo nje kidogo ya Jiji la Dares Salaam, hali ya afya ya Dk Ulimboka
imekuwa tete na jana ilizidi kuwa mbaya.
SOURCE THIS DAY MAGAZINE
SOURCE THIS DAY MAGAZINE
No comments:
Post a Comment