Katika hali ya kushangaza, maiti ya kichanga kilichozaliwa kikiwa
tayari kimefariki, imeyeyukia katika Hospitali ya Mwananyamala ya jijini
Dar es salaam, ambako mama aliyejifungua alikuwa amepelekwa kujifungua.
Kwa mujibu wa maelezo kuhusu kashfa hii ya aina yake, mama
aliyepoteza mtoto wake, alifika hospitalini hapo baada ya kushikwa na
uchungu ambapo alijifungua salama, lakini kwa bahati mbaya mtoto huyo
hakuwa riziki, na alishafariki.
Mama mzazi akakubaliana na maumivu ya uchungu pamoja na hali halisi
kuwa maandiko ya Allah yalishatimia. Lakini wauguzi katika Hospitali ya
Mwananyama wakaona kuwa vipigo hivyo havijamtosha mwanamke wa watu,
wakaamua kufunga kazi kwa kuupotezea kusikojulikana mwili wa kichanga
chake.
No comments:
Post a Comment