Kwa
mujibu wa mtandao wa Jamii Forums Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa
sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka
kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja
aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa
akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka
aonane naye face to face kwa ajili ya mazungumzo.
Dokta huyo aliokotwa akiwa na hali mbaya sana na hawezi kuzungumza.
Tukio
hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao
hata hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja,
kwani maeneo mengine yote huduma zimeendelea kama kawaida, isipokuwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Madaktari
hao wametangaza mgomo usio na kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali
kutimiza mahitaji yao, ikiwemo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi
pamoja na kuwapandishia mishahara.
Licha
ya mgomo huo kuanza kuleta madhara kwa wagonjwa katika siku ya kwanza
juzi, kwa madaktari kutofanya kazi katika hospitali mbalimbali nchini,
jana hali hiyo ilikuwa tofauti kwani sehemu nyingi huduma ziliendelea
kutolewa kama kawaida.
SOURCE THIS DAY MAGAZINE
No comments:
Post a Comment