Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 27, 2012

Madhara ya Mgomo Wa Madaktari Tanzania..


                                  Hii ni wodi ya wamama wajawazito Sekou Toure
                            Nani alaumiwe kwa hali hii...
 Mgomo wa madaktari katika hospitali za serikali nchini umeingia siku ya tano huku Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ikimwamuru Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Namala Mkopi, awatangazie madaktari hao wasitishe mara moja mgomo huo.

Jaji wa Mahakama hiyo, Lusekela Moshi, ametoa amri hiyo jana na kueleza kuwa Rais wa MAT anatakiwa kuwatangizia madaktari kupitia vyombo vya habari wasitishe mgomo huo hadi Julai 24, mwaka huu siku ambayo kesi ya madaktari itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
 Alisema jalada linalowataka madaktari kusitisha mgomo tayari limekwisha kupelekwa kwa Rais wa MAT Jumatatu wiki hii na kwamba kinachosubiri ni rais huyo kuwajulisha wananchama hao wasikaidi amri ya mahakama.

Jaji Moshi alisema mahakama inamtambua Rais wa MAT kuhusika katika mgomo huo kwa sababu awali alisikika akizungumza na vyombo vya habari kwamba madaktari watagoma.

No comments:

Post a Comment