Juma Jabu |
KLABU
tano za Ligi Kuu ya Tanzania zimewasilisha Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) majina ya wachezaji ambao zimewakatishia mikataba/mikataba yao
kumalizika au kuwaacha kwa ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa
2012/2013.
Kwa
mujibu wa klabu hizo, wachezaji waliomaliza mikataba Simba kwa mujibu
wa klabu hiyo ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago, Juma Jabu
wakati Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka
huu, wakati wachezaji ambao inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab
Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina.
Polisi
Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania
Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11.
Azam imekatisha mikataba ya wachezaji watatu.
Wachezaji
12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar wakati wakati
kwa upande wa Simba wachezaji waliomaliza mikataba ni wanne huku
ikionesha nia ya kuwatoa kwa mkopo wengine wanne.
Uhamisho
wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika
Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa
Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment