Hatimaye leo
mchana mchezaji wa zamani na nahodha wa klabu ya Simba Selemani Matola
amejiunga rasmi na klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam kama bosi wa
benchi la ufundi.
Matola ambaye
pia alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba amejiunga na klabu hiyo
ambayo kwenye msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja.
Mchezaji huyo
wa zamani wa Simba anaenda African Lyon kuchukua nafasi iliyoachwa wazi
na kocha aliyetimuliwa Jumanne Chale ambaye aliiongoza timu hiyo msimu
uliopita.
No comments:
Post a Comment