Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 12, 2012

HATIMAYE AFRIKA MASHARIKI YATOA MCHEZAJI LIGI KUU YA ENGLAND.


Ni mzaliwa wa Burundi lakini alihamia England kama mkimbizi yeye na familia yake kukimbia vita nchini mwao, na sasa anatumikia uraia wa Rwanda na anaichezea timu ya taifa ya nchi hiyo. Kwa jina anaitwa Gael Bigirimana aliyenyoa kijogoo ambaye alikuwa akiichezea klabu ya daraja la kwanza England inayofahamika kama New Coventry city ambapo alikuwa akiteremsha mvua ya magoli kwenye lango la wapinzani, Lakini kwa sasa mchezaji huyu anaweka historia kwenye
nchi za A.Mashariki kwa kuwa mchezaji pekee anayecheza ligi kuu ya England baada ya kusajiliwa na timu ya Newcastle kwenye msimu ujao wa ligi kuu na sasa wapinzani wategemee mvua ya magoli kutoka kwa kijana huyu mwenye umri wa miaka 18 anayechezea nafasi ya kiungo na mshambuliaji

No comments:

Post a Comment