ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE
- NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha miaka
100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya
Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha Yetu ni Huduma Bora
za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika tangu
tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kutakuwa na maonyesho yatakayoenda
sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakotembelea
mabanda yaliyoandaliwa.
Uchunguzi wa afya kama vile Kisukari,
moyo, shinikizo la damu, upimaji wa VVU, uchunguzi wa saratani ya
matiti kwa akina mama, huduma za macho na uzazi n.k zitatolewa kwa
kushirikiana na wataalam wa ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment