Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 5, 2012

Mashairi ya Fid Q yamkuna mhadhiri wa chuo kikuu



Na Joseph 'Josefly' Muhozi
Mhadhiri (lecturer) wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino ama SAUT, Mwanza,  ameguswa na mashairi ya ngoma ya Fareed Kubanda a.k.a Fid Q yaliyopo kwenye ngoma yake MWANZA MWANZA.
Denis Mpagaze, mtaalam wa masomo ya journalism and communication research, mwandishi wa vitabu na journals mbalimbali na mjuzi wa mambo ya falsafa, amewashangaza wanafunzi wake ambao wamezoea kukuta matangazo mbalimbali kwenye page yake ya facebook yanayohusu masomo na quotation za waandishi maarufu wa vitabu.
Tofauti na siku zote, wanafunzi wake wamekutana na maandishi yanayosema, “‘‘USIJARIBU KUPIMA KWA SHINGO UKALI WA UPANGA AU KUIMBA UNAKULA KARANGA NA SUMU KWA KUILAMBA...MANENO NI MKUKI, HEKIMA NGAO... (FID Q)
Kitendo cha mhadhiri huyo kukubali uandishi wa Fid Q, unadhihirisha jinsi mashairi yake yalivyotukuka, hata ukizima beat na snare bado maneno anayotumia yanaweza kupenya na kugusa vichwa kama hivi katika vyuo vikuu.
Mwenyewe Fid Q aliwahi kusema, ‘nasikika hata ukini-mute.’
Kutokana na status ya mhadhiri huyo, maswali kibao yalizuka, “Kumbe unapenda mistari ya wana hip hop sir? Aliuliza dada mmoja anaeitwa Neema Nyange.
Na mwingine aitwaye Deogratias Konyani alisema, ‘Dah! Falsafa za kitaaolojia by Fid Q! Hip hop unaipenda sir?’ huku Maulid Mombo naye akiungana na wenzie kuuliza,’Dah ticha umenifurahisha kumbe na we umo safi bt umesikia kitu kipya cha fid q-Sihitaji rafiki ?’ na Garma Paul kuchangia, ‘ticha we mwana hip hop nini?’
Kutoka na maswali hayo, mhadhiri huyo akajibu kwa kusema, ‘Namaanisha kimaisha, kwenye fani ukiwa na akili unatoka vizuri sana na haraka, kwenye vitabu hata uwe committed kiasi gani unakuja kutoka uzeeni’
Does this mean huyu mwalimu anatamani kuingia kwenye game ili afikishe alichoandika kwenye vitabu kwa wahusika haraka zaidi? I can’t tell, ila alikili kuwa anayo album ya Fid Q tayari mkononi na ili kudhihirisha kuwa anayajua mashairi kibao ya NGOSHA aliandika, ‘Akupigaye ngumi ya jicho na we mpige ya sikio, akikuuliza unaonaje na we muulize unajiskiaje.....ni vigumu majivu kuwa mkaa..’

No comments:

Post a Comment