*WADAU KUMRADHI KWA PICHA IFUATAYO HAPO CHINI KAMA ITAWAKWAZA.*
Mtoto
mchanga aliyezaliwa akiwa hana mikono, kifua, shingo na kichwa, ila
ana anasehemu ya miguu , makalio na tumbo akiwa katika hospitali ya mkoa
wa Singida muda mfupi baada ya kuzaliwa na Bi. Amina Bilau mkazi wa
kijiji cha Mtamaa tarafa ya Mwakonko manispaa ya Singida. (Picha na
Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mtoto mchanga amezaliwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiwa hana baadhi ya sehemu za mwili kuanzia kifuani hadi kichwani.
Kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dkt. Joseph Malunda,
amesema hospitali ya mkoa wa Singida ni mara ya kwanza kuzaliwa kiumbe
kama hicho tangu kuwa hospital ya mkoa.
Dkt.
Malunda amesema watoto hao ambao wamezaliwa mapacha wote wa kike wakiwa
na miezi saba, mmoja ambaye ana viungo vyote alikuwa na kilo 1.3
lakini alifariki baada ya saa sita kupita.
Dkt.
Malunda amesema baada ya mama mzazi wa watoto hao Amina Bilau
kujifungua mtoto wa kwanza, waliona mtoto mwingine akifuatia na ndipo
alipojifungua kitoto hicho chenye kilo 1.4 ambacho hakina mikono
,kifua,na kichwa
Kutokana
na hali hiyo Dkt. Malunda amewashauri wakina mama wanapopata uja uzito
kuhudhuria kliniki na kuacha kutumia madawa makali pindi wanapokuwa
wajawazito.
Dk.
Malunda amesema madawa ya aina hiyo yanaweza kuchangia kwa kiasi
kikubwa kuzaliwa watoto ambao wanakuwa na mapungufu ya viungo.
Akieleza
huku akiwa amelazwa katika hospita ya mkoa wa Singida mama huyo Amina
Bilau ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtamaa kata ya Mwankoko Manispaa
ya Singida, amesema yeye aliona tumbo lina kuwa kubwa na baada ya
kupata matibabu katika zahanati ya kijiji bila mafanikio aliamua kwenda
katika hospita ya mkoa wa Singida na kijifungua watoto akiwa katika
hali hiyo.
Kwaupande
wake baba wa watoto hao Maulidi Mkuki alipohojiwa, amesema anashangaa
kuona mke wake amejifungua mtoto wa aina hiyo wakati yeye ana watoto
wengine watatu ambao wamezaliwa bila ya kuwa na matatizo yo yote.
Katika
hatua nyingine wagonjwa walio fika kutibiwa katika hospitali ya mkoa wa
Singida mchungaji wa kanisa la Anglikana Harodi Ibuku na mkazi wa
Singida Atanas Malya, wamesifu madakta kuendele kutoa huduma.
Wamewashauri
kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete baada ya kuhutubia Taifa na kuwataka
kusitisha mgomo na kuendelea kutoa huduma ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Habari kwa Hisani ya Mo Blog
Habari kwa Hisani ya Mo Blog
No comments:
Post a Comment