Takriban watu 30 wamefariki dunia
baada ya meli iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya mia mbili na hamsini
kuzama karibu karibu na kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania .
Kwa mujibu wa taarifa zilizitolewa na
kikosi cha wanamaji, watu wengine wengi wanaripotiwa kuokolewa kufuatia
meli hiyo kuzama kutokana na dhoruba kali.
Mmoja wa watu waliofika katika eneo
kulikotokea ajali hiyo na kushiriki katiia uokoaji ni Mohammed Omar
ambaye aliambia BBC kuwa meli hiyo ilikuwa imepinduka na injini zake
zikiwa juu: "wengi wa waliookoka ni wale wanaojua kuogolea vivi hivi na
Mwenyezi Mungu."
Mwandishi wetu wa Dar Es Salaam,
Hassan Mhelela, ambaye amekuwa akifuatilia ajali hiyo tangu itokee jana
amesema shughuli za uokoaji zimeripotiwa kuanza tena.
Alisema zilisimamishwa jana usiku kwa sababu ya hali mbaya ya bahari na giza.
Mwaka mmoja haujakamilika tangu
kutokea ajali nyingine kutoka katika njia hiyohiyo ya meli na
kusababisha vifo vya mamia ya watu.
No comments:
Post a Comment