Baadhi ya vitu vya mwanachuo vilivyokuwa vimeibiwa na kibaka (aliyefungwa pingu).
Wanausalama wakiorodhesha vitu vilivyokutwa kwa kibaka huyo.
Joseph Chillo akiwa chini ya ulinzi mkali.…
Baadhi ya vitu vya mwanachuo vilivyokuwa vimeibiwa na kibaka (aliyefungwa pingu).
Wanausalama wakiorodhesha vitu vilivyokutwa kwa kibaka huyo.
Joseph Chillo akiwa chini ya ulinzi mkali.
...Kibaka Joseph Chillo akielekea kwenye gari tayari kwa safari ya polisi.
...Joseph akipanda gari.
Kibaka huyo aliiba hadi madaftari ya chuo ya Evarist.
Mwanafunzi wa Chuo cha Ujenzi
mkoa wa Morogoro, Evarist Njogoro aliyeibiwa vitu vyote yakiwemo
madaftari ya chuo na Joseph Chillo.
KIJANA mmoja anayedaiwa kuwa kibaka ajulikanaye kwa jina la Joseph Chillo, mchana huu amekamatwa mtaa wa Lusongo katika kata ya Sabasaba mkoani hapa akidaiwa kuvunja chumba cha mwanafunzi wa Chuo Cha Ujenzi Morogoro, Evarist Njogoro na kumuibia vitu yakiwemo madaftari.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinadai kwamba Kibaka huyo alifanya wizi huo jana usiku kwenye mtaa maarufu kwa jina la Chaka Bovu na kuficha vitu hivyo kwenye nyumba moja iliyo jirani na eneo hilo.
"Mwanafuzni huyu ambaye alikwenda kujisomea kwa rafiki yake aliporudi alikuta chumba chake cheupe na kuanza kuangua kilio, sisi kama majirani tulibeba jukumu la kumsaidia kwa kuwa ni mgeni mkoani hapa, hivyo kwa uzito wa tukio hilo tulifanya upepelezi na kubaini kwamba vitu hivyo viliingizwa kwenye nyumba hii" alisema mmoja wa majirani wa mtaa huo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

No comments:
Post a Comment