Jarida
maarufu la kimarekani la Forbes leo hii limetoa tena listi ya vilabu
vya michezo yote vyenye thamani kubwa duniani, na kwa mara nyingine tena
pamoja na kutochukua kombe lolote msimu uliopita na kutolewa mapema
kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya Manchester United imeendelea kushika
usukani mwa vilabu tajiri duniani huku ikifuatiwa na Real Madrid.
Timu
nyingine za mchezo wa soka zilizopo kwenye Top 10 ni Barcelona
wanaoshika nafasi ya nane, huku Arsenal ya England ambayo haijchukua
kombe lolote kwa miaka inayokaribia kufikia nane ikishika nafasi ya 10,
wakiwazidi mabingwa wapya wa Ulaya Chelsea wanaoshika nafasi ya 45 huku
matajiri wa England Man City wakiwa hawapo hata kwenye Top 50. Timu
nyingine za soka zilizopo kwenye listi hiyo ni Bayern Munich wanashika
nafasi ya 11, AC Milan wanashika nafasi ya 27.
#1 Manchester United ($2.23 billion)
#3 New York Yankees ($1.85 billion)
#5 Washington Redskins ($1.56 billion)
#6 New England Patriots ($1.4 billion)
#9 New York Giants ($1.3 billion)



No comments:
Post a Comment