Polisi
wa Kenya wanasema kuwa wanaendelea na uchunguzi, juu ya mauaji ya
balozi mpya wa Venezuela nchini humo, ambaye aliuwawa Ijumaa.
Olga
Fonseca, aliyeanza kazi Kenya kati ya mwezi Julai, alikutiakana
ameuwawa nyumbani kwake, na watu sita wamekamatwa hadi sasa.Watu hao
sita wamekamatwa siku mbili tu baada ya balozi huyo kupatikana amefariki
nyumbani kwake.
Siku
ya Ijumaa, polisi walisema kuwa maiti ya Bi Olga Fonseca ilipatikana
kitandani mwake lakini sababu za kuuwawa kwake hadi sasa hazijulikani.
Bila
ya kutoa maelezo zaidi, polisi wamesema kuwa wanawashikilia watu sita
kuhusiana na kifo cha balozi huyo.Taarifa kutoka wizara ya maswala ya
njee ya Kenya imesema kuwa wafanyikazi katika makaazi ya balozi huyo
waliwasilisha malalamiko yao kwa polisi baada ya kufutwa kazi hivi
majuzi.
Inadaiwa
kuwa bi Fonseca aliwafuta kazi baada ya wao kukataa kuondoa malalamiko
kuhusu madai ya kunyanyaswa kijinisia na mtangulizi wa balozi huo.Hata
hivyo polisi wamesema wanachunguza madai hayo
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili
No comments:
Post a Comment