Rais Obama ameelezea mafanikio waliyonayo ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha
ukosefu wa ajira kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miaka mitano kufufua Sekta ya nyumba na makazi utengenezaji
bidhaa zinazobuni nafasi za ajira na kuzalisha mafuta zaidi ndani ya Nchi .
Aidha Rais Obama ameongeza kuwa licha ya kushuhudia miaka minne ya ukuaji wa uchumi na
faida kubwa iliyovunwa na makampuni, ukosefu wa usawa umezidi kukita mizizi nchini marekani
Sanjari na hayo ameongeza kuwa yupo tayari kuendelea kufanyakazi na wabunge
wa Bunge la Congress ili kurekebisha baadhi ya mambo lakini hatasita kuchukua hatua za kurekebisha mambo yanayotokea
ndani ya bunge hilo hata bila marekebisho ya sheria kupitia Congess.
No comments:
Post a Comment