Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 1, 2012

MBUNGE WA NKASI KASKAZINI, ALLY KESSY 'AIBUKA MSHINDI WA KUTUMIA BASTOLA KWA KULENGA SHABAHA




Mhe. Ali Kessy, Mbunge wa Nkasi Kaskazini.

Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia CCM, Mhe. Ali Mohamed Kessy, ameng’ara katika shindano maalum la kulenga shabaha kwa matumizi ya bastola na kuwamwaga wapinzani wake, wakiwamo waheshimiwa Mathayo David, Martha Mlata na David Silinde.

Akizungumza bungeni jana, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai alisema kuwa, Mhe. Kessy, alionyesha umahiri mkubwa katika shindano hilo lililowashirikisha waheshimiwa wabunge kwa kulenga shabaha kwa kutumia bastola na bunduki, lililofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki na kuibuka kidedea katika shindano hilo.

Washindi wengine waliotangazwa bungeni jana katika shindano la kulenga shabaha ni pamoja na Waziri wa Ushirika na Masoko, Mhe. David, ambaye yeye aliibuka kidedea katika kutumia bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) huku Mhe. Mlata akishika nafasi ya pili katika kulenga shabaha kwa kutumia bunduki aina ya Light Machine Gun (LMG).     

Wakati Mhe. Ndugai akimtangaza Kessy, kuwa ndiye mshindi katika kulenga shabaha kwa bastola, ukumbi mzima wa bunge uliripuka kwa shangwe, vicheko na nderemo.

No comments:

Post a Comment