Na Mwandishi Wetu,Arusha.
IDARA
ya Uhamiaji mkoani Arusha, inamshikilia mtu mmoja anayehusishwa na
biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu waliokamatwa katika Msitu wa
Chitego, Dodoma ambapo miongoni mwao 45 walipoteza maisha kwa kukosa
hewa katika lori walilokuwemo.
Habari
zilizopatikana zinaeleza kuwa mtu huyo (jina linahifadhiwa), amekuwa
akifanya biashara hiyo kwa kusafirisha wahamiaji kutoka Ethiopia na
Somalia kupitia nchini kwa muda mrefu.
Hata
hivyo, taarifa zinadai kwamba tayari kumekuwa na njama za chini kwa
chini zinazosukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya maofisa wa idara hiyo
mkoani hapa, kutaka kumwachia mtuhumiwa huyo.
Kukamatwa
kwa raia huyo kumekuja wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini,
Pereira Ame Silima akisema kwamba kitendo cha kusafirisha wahamiaji
haramu nchini kimekuwa ni mchezo wa kawaida, kwani Watanzania ndiyo
wanaowasaidia kuwasafirisha kutoka Nairobi kupitia Arusha na mara nyingi
hupita usiku katika njia za panya.
Vyanzo
vya habari vimelieleza gazeti hili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni raia
wa nchi jirani ya Kenya alikamatwa Juni 25 mwaka huu wilayani Longido
akiwa katika harakati za kusafirisha wahamiaji haramu wengine kutokea
nchi jirani ya Kenya.
Vyanzo hivyo vimedai kuwa mtuhumiwa huyo mara baada ya kukamatwa al
ifikishwa moja kwa moja katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha huku lori alilokuwa ndani yake likipotea katika mazingira ya kutatanisha.
ifikishwa moja kwa moja katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha huku lori alilokuwa ndani yake likipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Vyanzo
hivyo, vilienda mbali zaidi na kubainisha kwamba mtuhumiwa huyo na
washirika wake wamekuwa wakilipwa Dola3,000 za Marekani kwa kila raia
wanayemsafirisha ambapo kazi hiyo imekuwa ikiwashirikisha baadhi ya
vigogo wa Idara ya Uhamiaji.
“Wamekuwa
wakilipwa Dola 3,000 kwa kila kichwa, kazi hiyo inafanywa kwa umakini
mkubwa na hata maofisa wa uhamiaji wanahusika, kwa mfano wakiwa njiani
wanawasafirisha hao wahamiaji haramu, endapo ikigundulika kwenye lori
kuna mtu kafa anamweka chini ya gari na kukanyagwa ili ijulikane
aligongwa na gari kupoteza ushahidi,” kilisema chanzo.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini ya kwamba baadhi ya maofisa wa
uhamiaji mkoani hapa waliwaambia washirika wa mtuhumiwa huyo kwamba
wanapaswa kutoa Sh40 milioni ili aweze kuachiwa kitendo kilichozua
mabishano makali baina ya pande mbili.
Pia
uchunguzi huo umebaini ya kwamba mara baada ya mabishano hayo washirika
hao waliomba kupunguziwa kiasi hicho cha fedha na ndipo maofisa hao wa
uhamiaji waliwaambia watoe Sh25 milioni kitendo kilichoafikiwa na pande
mbili.
Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha, Daniel Namomba alikiri taarifa za
kushikiliwa kwa raia huyo na kusema kwamba wamemshikilia akiwa na
wenzake watatu.
Lakini alikanusha madai ya kutaka kuachiwa kwa njia za rushwa na kusisitiza kwamba bado wanafanya uchunguzi.
“Ni
kweli tunamshikilia, wako wanne jumla na bado tunalifanyia kazi
tukikamilisha uchunguzi tutakupeni taarifa kamili, sisi hatujabaini
chochote kuhusu tuhuma za rushwa,” alisema huku akikataa kutaja sababu
ya kukamatwa kwa raia hao.
Hata
hivyo, uchunguzi wetu ulibaini kuwa washirika hao walikuwa na Sh20
milioni na walikuwa wakizunguka jijini Arusha kwa kutumia gari aina ya
Noah wakifanya juhudi za kujazia Sh5 milioni ili kukamilisha kiasi chote
na kukiwasilisha mbele ya maofisa hao.
Kaimu
mkuu wa idara hiyo mkoani hapa, Johannes Msumule alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo huku akikataa kulizungumzia kwa undani kwa madai kwamba
suala hilo ni nyeti na linashughulikiwa na vyombo mbalimbali vya usalama
nchini.
Wakati
huo huo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani
hapa chini ya Kamanda wake, Mbengwa Kasumambuto ameliambia gazeti hili
kwamba wamejitosa kuchunguza tukio hilo baada ya kupokea taarifa za
wingu la rushwa kutanda ndani ya sakata hilo.
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment