Messi wa Msimbazi; Rama Singano |
KIUNGO
chipukizi wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’ anatarajiwa kuondoka
nchini wakati wowote kwenda Austria kwa majaribio ya soka ya kulipwa,
imeelezwa.
Chanzo
cha habari cha uhakika kutoka ndani ya Simba SC, kimesema jana kwamba,
Messi amepata ofa hiyo ya majaribio kupitia wakala mmoja wa wachezaji
Tanzania, anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),
anayefanya kazi na klabu hiyo.
“Kuna
wakala mmoja ambaye anafanya kazi na sisi, ameleta ofa hiyo na kama
kijana atafuzu, Simba itapata kama dola za Kimarekani 300,000
hivi,”kilisema chanzo kutoka Simba SC.
Messi
huyo alipandishwa kutoka timu ya vijana ya Simba msimu uliopita na
pamoja na kuingia mara chache akitokea benchi, lakini amewavutia wengi
kwa soka yake na kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Tayari
mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, anaendelea na majaribio katika
klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Austria yenye maskani yake
Wals-Siezenheim, nchini humo na baada ya hapo ndipo majibu yatatoka.
Klabu
hiyo inayotumia Uwanja wa Red Bull Arena, ikiwa zaidi inafahamika kama
SV Austria Salzburg kabla haijanunuliwa na kampuni ya Red Bull mwaka
2005, imewahi kufika Fainali ya Kombe la UEFA mwaka 1994 na inacheza
Ligi Kuu ya Austria, iitwayo Bundesliga kama Ligi Kuu ya Ujerumani.
Timu
hiyo ni kama timu ambayo Okwi, anachezea kwa sasa, Simba SC, kwani nayo
inavaa jezi za rangi ya nyeupe na nyekundu na imewahi kutwaa taji la
Bundesliga ya Austria mara saba na pia ilicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
msimu wa 1994–1995 kama Casino Salzburg, na kuwa timu pekee, ambayo
haikufungwa na mabingwa wa wakati huo, Ajax Amsterdam.
Awali,
Okwi aliikosesha Simba Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya
Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini na kuamua kwenda Austria, ambako
inaelezwa klabu hiyo iko tayari kutoa Euro 600,000 akifuzu.
Awali
Orlando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko
kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa
taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
Hata
hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza
Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu. Wakala
aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka
Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini
bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi
Kuu ya Afika Kusini (PSL).
SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment