Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wa Mkoa wa Kimichezo wa
Kinondoni,Salum Dosi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa uzinduzi wa mashindindano ya Safari Pool Taifa kwa Mikoa mitatu ya
kimichezo, Kinondon,i Temeke na Ilala Dar es Salaam jana.Katikati ni
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Katibu wa Chama cha
Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wa Mkoa wa Kimichezo wa
Kinondoni,Salum Dosi akimkabidhi t-shirt mwakilishi wa Klabu ya Jaba wa
Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Mayaula Muhagama wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya Safari Pool Taifa kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambao
unajumuisha mikoa mitatu ya kimichezi, Kinondoni ,Ilala na Temeke jana.
Mchezaji wa Safari Pool Taifa wa Klabu ya East London Mkoa wa
kimichezo wa Temeke , Amos Boniphace akicheza kuashilia uzinduzi
mashindano hayo Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mchezo wa pool yanayojulikana kama 'Safari Lager
National Pool Championship 2012' katika mikoa maalum ya kimichezo ya
Temeke, Ilala na Kinondoni yameanza kutimu vumbu leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa uzinduzi wa
mashindano hayo, katibu mkuu wa chama cha mchezo huo nchini (TAPA),
Amosi Kafwinga alisema kuwa maandalizi yote katika mikoa hiyo tayari
yamekamilika.
Kafwinga alisema kuwa klabu 10 kutoka Temeke, 12 Kinondoni na 12
Ilala zitachuana vikali katika mashindano hayo ngazi ya mikoa ambayo
yanadhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.
Alisema kuwa bingwa wa kila mkoa licha ya kuzawadiwa fedha taslim
Sh.700,000 lakini pia atakata tiketi ya kushiriki fainali za taifa za
mashindano hayo zitakazofanyika Septemba mkoani Mwanza.
Naye meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema kuwa wao
kama wadhamini tayari wamekamilisha kila kitu kinachohusiana na
mashindano hayo ikiwa ni pamoja T-shirt na pesa za maandalizi kwa timu
zote.
Shelukindo alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha mchezo huo unaenea
nchi nzima hasa ikizingatia mwaka jana yalishirikisha mikoa 14 lakini
mwaka huu yanashirikisha mikoa 16.
Makamu mwenyekiti wa Baraza la Michezo Wilaya ya Kinondoni, Salim
Dossi ambaye ndiye aliyekabidhi T-shirt pamoja na pesa za maandalizi kwa
timu zote, aliwapongeza wadhamini wa mashindano hayo bia ya Safari
Lager kwa kuweza kuinua mchezo huo nchini.
Dossi aliwataka wadhamini hao kutouacha mchezo huo bali waendelee na
juhudi zao za kuudhamini ili nao uweze kuwa moja ya michezo tishio kama
ilivyo soka kutokana na kwamba tayari dalili zimeanza kuonekana.

No comments:
Post a Comment