WAKAZI wa
Temboni Mtaa wa Kimara ‘B’ na Upendo jijini Dar es Salaam, wameliomba
jeshi la polisi, kutoa ushirikiano wa dhati katika kupambana na wimbi la
majambazi lililoshamiri maeneo hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Diwani wa Kata ya Saranga Efraimu Kinyafu
(Chadema),alieleza kuwa awali maeneo hayo yalikuwa na matukio ya
ujambazi wa kutisha ambao ulisababisha baadhi ya watu kupoteza maisha
yao huku wengine wakipata ulemavu.
Alichanganua
kuwa kutokana na wimbi hilo la majambazi mwaka 2010 hadi 2011 jeshi la
polisi kwa ushirikiano wa wananchi liliweka askari wa doria kwa masaa
24 ambao kwa pamoja walifanikiwa kutokomeza majambazi hao ila kwa sasa
wimbi hilo limejitokeza kwa mara nyingine tena.
“Majambazi
hao wameanza kujitokeza tena katika maeneo ya upendo, kimara, temboni
maduka saba, na wanatumia silaha vikiwemo vitu vyenye ncha kali kwa
kuvamia maduka na kupora fedha pamoja na kuacha madhara mbalimbali kwa
wananchi.
Hata hivyo,
diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwataka askari polisi wa kituo cha
Mbezi Luis kuwa makini katika kutekeleza kazi zake badala ya kuwa chachu
ya kusababisha vifo kwa wananchi wasiokuwa na hatia.
Mbali na
hilo diwani huyo alidai kuwa askari polisi waliopo kwa sasa katika kituo
hicho hawana ushirikiano kama walivyokuwa awali,kwani wamekuwa
wakiwashinikiza wananchi kutumika kama askari wa ulinzi shirikishi.
“Katika hili
kuna baadhi ya uzembe unafanywa na kituo hicho, mfano hivi karibuni
kuna kijana mmoja mwendesha bodaboda alipoteza maisha yake baada ya
kujigonga katika nguzo ya umeme wakati akiwakimbia polisi waliokuwa
wakimfukuza wakimshuku kuwa ni mhalifu alifafanua Kinyafu.
Naye Kamanda
wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charlrs Kenyela alishangazwa na tukio la
kijana huyo ambalo hadi sasa halijafikishwa ofisini kwake, ila akahaidi
kutoa ushirikiano pindi taarifa hizo zikiwasili kwake.
“Aksante kwa
taarifa hizo, na ieleweke kuwa kimara ni eneo lenye wakazi wengi na
matukio ya ujambazi zi leo kwa sababu hata miaka miwili ya nyuma
walikuwepo ila nawaahidi wakazi wa eneo hilo kushirikiana nao bega kwa
bega katika kuwatokomeza, kwa mujibu wa Kenyela


No comments:
Post a Comment