Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 5, 2012

Shirika laonya baa la njaa Somalia



Mtoto mgonjwa anayekabiliwa na tishio la kuangamia nchini SomaliaShirika la Save the Children, limeonya kuwa ukosefu wa mvua ya kutosha na kuendelea kwa mzozo nchini Somalia, kunatishia kusambaratisha mafanikio yaliyoafikiwa tangu mwaka uliopita, wakati taifa hilo ilipokumbwa na baa la njaa.
Shirika hilo limesema ikiwa hali hiyo itaendelea, maisha ya maelfu ya watoto imo hatarini.
Shirika hilo la save the children, limesema idadi kubwa ya familia nchini Somalia, hawana uwezo wa kukabiliana na athari za ukame na kutoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi ya dharura nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment