Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. |
Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika leo Dar es Salaam baina ya shirika hilo na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambapo hali hiyo ilielezwa kuwa moja ya hatua zinazofanywa na NHC katika kutafuta mitaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi.
Taasisi za fedha zilizotoa mkopo huo pamoja na kiwango walichotoa kwenye mabano ni pamoja na CRDB (Sh bilioni 35), ECO Bank (Sh bilioni 2), TIB (Sh bilioni 22), BancABC (Sh bilioni 4.2), NMB (Sh bilioni 26), CBA (Sh bilioni 24), LAPF (Sh bilioni 15), Azania (Sh bilioni saba) na Shelter Afrique (Sh bilioni 23).
No comments:
Post a Comment