Derrick Walulya mchezaji wa timu ya URA FC kutoka nchini Uganda ambaye
aliwahi kuchezea timu ya Simba pia ya Tanzania akimiliki mpira mbele ya
Felix Sunzu mshabuliaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kuwania kombe
la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika
Mashariki CECAFA unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni hii mpaka sasa
ni kipindi cha pili na timu ya URA inaongoza goli 1-0 dhidi ya Simba.
Waamuzi wakiongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na
URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja
wa Taifa jioni hii.
Watangazaji wa kituoa cha televisheni cha Supersport cha Afrika Kusini
wakitoa tathmini ya mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana ambapo
inaonyesha kuwa Simba mara nyingi imekuwa ikifungwa na URA FC wakati
timu hizo zinapokutana katika michuano mbalimbali.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika katika uwanja wa Taifa kujionea timu yao ikicheza na Waganda URA FC.
No comments:
Post a Comment