SHUJAA WA SIMBA; Christopher Edwar |
SIMBA
SC jioni imepata ushindi wa kwanza katika michuano ya BancABC Sup8r
kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, baada ya kuifunga Mtende FC ya
Zanzibar mabao 2-0.
Simba,
ambayo kwenye mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya 1-1 na Jamhuri ya
Zanzibar pia, mabao yake katika mchezo wa leo yalifungwa na Christopher
Edward dakika ya 11 na 26 kwa penalti.
Mtende
walilazimika kumaliza pungufu mechi hiyo, baada ya mchezaji wake, Rajab
Mzee kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 86 kwa kumtolea lugha
chafu refa wa kike, Judith Gamba.
Simba
inatumia kikosi chake cha pili kwenye mashindano haya, ambacho kipo
chini ya kocha Suleiman Abdallah Matola, Nahodha wa zamani wa Simba SC.
Katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam walifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mabao yote ya Mtibwa yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji wakiwa ni Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Hussein Javu.
Mtibwa
iliyoifunga Polisi Moro 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, sasa inaongoza
kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi tatu,
ambayo katika mchezo wake wa kwanza, iliifunga Super Falcon 2-0.
NA BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment