Shirika
la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International,
linasema limeambiwa kwamba Gambia imewanyonga wafungwa tisa kati ya 47
ambao wamehukumiwa kifo.
Tumepata
taarifa za kuaminika kuwa watu 9 walinyongwa jana usiku.Msemaji wa
Amnesty, Lisa Sherman Nichols, alisema kwamba wafungwa hao ni wa mwanzo
kunyongwa nchini Gambia kwa miaka 29, na inasemekana alikuwako mwanamke
kati yao, na wananchi watatu wa Senegal.
Nimezungumza na baadhi ya jamaa zao, ambao bila ya shaka wako kwenye majonzi, na wametuomba tuchukue hatua.
Wamegusia kuwa kuna wengine watanyongwa leo usiku.
Tunajaribu
kuzitawanya habari hizi ulimwenguni na serikali ya Gambia inafaa kujua
kuwa macho ya ulimwengu na serikali za nchi za nje yameelekezwa juu ya
nchi hiyo."
Hapo
awali, shirika la raia la nchi hiyo lilimlaumu rais wa Gambia, Yahya
Jammeh, na lilisema kwamba wengi waliohukumiwa kifo ni wafungwa wa
kisiasa.
No comments:
Post a Comment